Aug 31, 2012

Tourist guides training programme

From L-R: Mr Gonzalez, Pd Miguel and Mwl George, the brains behind the 'tour guides training programme

Started nearly a year ago, the programme have seen some inspired six young men becoming the first of the indigenous Hadzabe to qualify as tourist guides. The six have been trained in basic guiding skills, English language and the geography of the area. These six guides have all passed their examinations and are now working freelance, as we as CBO, are working to get our programme running.

Another group of six students are now in training, with, for the first time, inclusion of girls. This second group will complete their studies in December this year thus equipping the community with twelve trained tourist guides.

Aug 29, 2012

Risala ya siku ya Mahafali


A group photo of the graduands, sponsors Mr. Gonzalez & Pd Miguel and other civic leader 


Ifuatayo ni risala ya Wanajamii waliyoisoma siku ya mahali ya vijana waliohitimu mafunzo ya kuongoza watalii (tour guides)


RISALA FUPI YA JAMII YA WAHADZABE WA MANG’OLA KATIKA MAHAFALI YA VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO YA KUONGOZA WATALII, TAREHE 14 JULAI 2012.

Ndugu Mgeni Rasmi,

Ifuatayo ni risala fupi ya wana asasi ya jamii ya Wahadzabe wanaoishi katika bonde la ziwa Eyasi inayosomwa mbele yako katika mahafali ya vijana wa Kihadzabe wanaohitimu mafunzo ya kuongoza watalii (tour guides).

Ndugu Mgeni Rasmi,

Tuanze kwa historia fupi ya jamii hii. Jamii ya Wahadzabe ni jamii pekee iliyobaki duniani ambayo bado watu wake wanaishi kwa kutegemea uwindaji na ukusanyaji wa matunda na mizizi kama ilivyokuwa miaka elfu nyingi iliyopita. Tumekuwa tukiishi katika Bonde la ziwa Eyasi kwa miaka mingi bila muingiliano na watu wengine kwa muda mrefu. Lakini tangu miaka ya 1990 tulianza kuona ujio wa wageni hasa watalii kutoka mataifa mbalimbali. Ingawa jambo hili linaweza kuonekana kama baraka, pia limeleta matatizo na lina changamoto nyingi kwetu kama jamii na namna tunavyoendesha maisha yetu. Kutokana na ongezeko kubwa la watu katika eneo hili la Mang’ola, tumejikuta tukinyang’anywa maeneo yetu ya asili tuliyokuwa tukiyategemea kwa ajili ya kujipata mahitaji ya kila siku yaani matunda, mizizi na wanyama pori. Hivyo tumejikuta tukitegemea utalii kama shughuli nyingine inayotupatia riziki.

Ndugu Mgeni Rasmi,

Ujio wa utalii pia ulileta watu binafsi ambao pamoja na kuwa hawakuwa Wahadzabe ambao walitumika kueleza habari zetu na kuwaongoza watalii katika maeneo yetu. Hali hii ilipelekea upotoshaji (hasa kuhusu mila na desturi zetu), unyonyaji, na kushindwa kufaidika kwa Wahadzabe. Wahadzabe walibaki kuwa kama ‘chombo’ (objects of interest) badala ya kunufaika na shughuli za utalii zilizokuwa zinafanyika katika maeneo yao. Hivyo tuliamua kuchukua hatua, kwa msaada mkubwa wa Kanisa Katoliki chini ya Miguel na Pepe, kuwapa mafunzo ya kuongoza watalii vijana wa Kihadzabe ili waweze kutoa huduma hiyo kwa watalii wanaotutembelea na kutaka kujua habari kuhusu maisha yetu, tamaduni zetu na mila na desturi zetu.

Ndugu Mgeni Rasmi,

Tungependa ifahamike kuwa juhudi hizi tulizozianza zina lengo la kusaidia jamii ya Wahadzabe kujikwamua katika lindi la umasikini na utegemezi – hatupendi kuendelea kuwa watu wa kuomba omba. Tunawaandaa vijana ili waweze kuwa chachu ya kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii yetu, ili jamii yetu iweze kujitegemeza na kuendelea kuwapo kwa vizazi vingi vijavyo. Kwa hiyo basi, tunaomba ushirikiano kati yetu na serikali. Na hatutakuwa tumekosea kama tukisema tunahitaji jicho na ulinzi wa serikali kwa namna ya kipekee zaidi kuliko hata watu wa jamii nyingine. Pia serikali itambue kuwa bado hatujapata eneo la kutosha kwa ajili ya mahitaji ya jamii yetu, na kulingana na uvamizi unaoendelea wa watu kutoka sehemu mbalimbali, tunahitaji la kupewa umiliki wa kisheria wa ardhi kwa jamii yetu kama haki yetu ya msingi.

Ndugu Mgeni Rasmi,

Tunatambua kwamba wewe umekuwa mmoja wa watu wanaotusaidia ili tuweze kufikia malengo yetu ya kujitegemea na kuwa na rasilimali watu wanaoweza kupanga na kuamua namna tunavyotaka kuendelea. Tunakushukuru wewe na washirika wako kwa kutusaidia kuwalipia ada ya masomo vijana hawa ambao watahitimu leo. Tunazitambua na kuzithamini jitahada zako na tunaahidi kuwa na sisi tutafanya yaliyo katika uwezo wetu kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya jamii nzima ya Wahadzabe. Tunaamini kuwa utaendelea kuwa nasi bega kwa bega katika safari yetu hii ya kujikomboa na kujiinua kwa kusaidia elimu ya vijana wetu, afya na ustawi wao kwa ujumla.

Ndugu Mgeni Rasmi,

Tunashukuru pia kwa ushirikiano tunaopata kutoka serikalini, hasa serikali ya Wilaya kwa kukubali kwao na kuridhia kusajili asasi yetu ya kijamii na Bodi ya Utalii kwa miongozo wanayotupatia kuhusiana na kuanzisha programu ya utalii wa kitamaduni (cultural tourism). Pia shukrani ziende kwa serikali ya kijiji kwa kutupatia eneo hili la ardhi tuliopo leo. Tunaomba ushirikiano huu uendelezwe kwa manufaa ya jamii nzima na taifa kwa ujumla.

Asante kwa kunisikiliza.

Risala hii imeandaliwa na jamii ya Wahdzabe wa Mang’ola na kusomwa kwenu na Witness Maweshi.