Jul 26, 2013

Tanzia

Marehemu Mzee Panda akiwa kwenye ofisi ya CBO siku chache kabla ya mauti yake.
CBO na jumuia nzima kwa ujumla imepata pigo. 

Mzee Yohana Panda, aliyekuwa mwenyekiti wa asasi na jamii kwa ujumla alifariki dunia tar baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mzee Panda ndiye aliyekuwa mwenyekiti aliyesimamia na kupambana hadi kufikia mahali CBO ilipo sasa -- kupatikana kwa eneo kwa ajili ya shughuli za asasi, kupatikana kwa jengo la kudumu la ofisi, kusomeshwa kwa vijana wa kiHadzabe ili kufanya shughuli za utalii na kadhalika. Mzee Panda alishughulika bila kuchoka wala kukata tamaa, akitembea na kuzungukia makambi ya Wahadzabe ili kuhamasisha malengo na shughuli mbalimbali za asasi na maendeleo ya jamii hii kwa ujumla. 

Wakati tukimkumbuka mzee wetu huyu na mambo mengi aliyoyafanya ili kusukuma mbele gurudumu la kutaka kuona jamii yetu inapata haki zake na kuthaminiwa, ni wakati muafaka basi kwa sisi tunaobaki kuendeleza yale ambayo mzee Panda alitamani yatokee -- umoja zaidi kati ya wanajamii, mwamko zaidi, na kufanya kazi zaidi ili kuweza kufikia maendeleo yetu kama jamii na kama mtu mmoja mmoja.

Apumzike kwa amani.

No comments:

Post a Comment